Friday, February 27, 2009

Hujui Kinorweji,

hupati uraia au

kibali cha kudumu

hapa Norway




Serikali ya zamani ya Waziri Mkuu Kjell Magne Bondevik ilipeleka mswada Bungeni (Stortinget) mwaka 2005 kuwa wageni wote waliopo nchini, kabla hawajapewa uraia wa Norway, au kibali cha kudumu cha kuishi (bosettingstillatelse) lazima wafanye kozi ya Kinorweji ya masaa 300. Bunge la Norway likapitisha mswada huo na kuwa lazima wageni wathibitishe ufahamu wa Kinorweji kwanza kabla ya kukubaliwa uraia au kibali cha kudumu cha kuishi. 

Hadi sasa wageni kiasi cha 41000 wanaotarajiwa kufanya kozi ya lazima ya Kinorweji. Ni 14000 tu waliomaliza kozi tokea 2005.

Serikali imeamua kuanzia sasa wageni wote ambao hawatathibitisha ufahamu wao wa Kinorweji hawatapewa uraia au kibali cha kudumu cha kuishi.

Mwaka huu, watu 4 wamekataliwa uraia wa Norway na 60 (mwaka huu pekee) wamerudishiwa fomu zao za kuomba uraia kwa kushindwa kuthibitisha ufahamu za Kinorweji.  Hayo yamesemwa na Bi. Cecilie Sande Amundsen wa idara ya uhamiaji (utlendingsdirektoratet = UDI, akiliambia gazeti la Aftenposten leo Ijumaa 27 Februari.

Wengi hawahudhurii kozi ya lugha ya masaa 300 kwa sababu ni ghali, inagharimu kroner 15000 (kuminatanoelfu)

Chanzo cha habari: Aftenposten, Ijumaa, 27 Februari 2009


2 comments:

Anonymous said...

Mama weeeeeeee!!!!! twafa....

Anonymous said...

Shauri yenu nyie mnaokaa huko Kaskazi ya Dunia....