Maswali na majibu
kuhusu sisi Watanzania
Na Dk. Kakoloboji K. Mwandanji (Gazeti la Rai) SWALI: Hivi ndugu yangu haya mambo yasiyo na kichwa humu taifani mwetu huwa yanapenyezwaje? Jibu: Najua bila shaka unaweza kuniambia ni yapi. Swali: Kwani wewe huyajui? Jibu: Hata kama najua baadhi, lakini wewe mtoa wazo nadhani unayajua mengi zaidi kuliko mimi. Swali: Mfano mmoja; nani alitoa wazo la kutaifisha shule za binafsi? Jibu: Wewe na mimi hakuna haja ya kumjua. Swali: Mfano wa pili; nani alitoa wazo kwamba shule ziruhusiwe kuwa za binafsi? Jibu: Rafiki yangu amenipa ka wisdom kwamba ukifukua fukua makaburi utakuta mle alimozikwa ndugu yako kuna gogo la mpingo. Swali: Unanitisha sio? Jibu: Ngoja tuongelee yaliyo rahisi. Swali: Nani alifuta benki kuwa za umma akasema zimezama kiholela? Nani huyo? Jibu: Ndugu yangu tafuta mambo ya maana na ambayo tunaona yanaeleweka. Swali: Usemavyo ni sawa. Lakini ni nani alitoa wazo la kuvuruga viwanda vyetu? Ee, nani huyo? Jibu: Tumwache huyo. Utakuta gogo la mpingo kama rafiki yangu alivyoniwizdomisha. Swali: Mbona basi barabara kwa mfano hazijapewa sifa ya kijasiriamali, kwa nini? Jibu: Wajasiriamali wapo kwenye kushughulikia vitu ambavyo haviingizi hela nzito. Wewe na mimi tujasiriemali ya kutilia, kusukuma guta au hata siku hizi ukopeshwe vijisenti ukavue samaki kwenye mto ulio karibu na kijijini kwenu. Nafikiri unaelewa. Swali: Madaktari walikuwa hawaruhusiwi kuganga njaa kwa kuwa na hospitali zao, siku hizi ruhusa ipo, je, pana utofauti kwa wananchi? Jibu: Ndio, wananchi wanateseka kumuaksesi mganga. Maana hapa pochi ni lazima. Uraia wako, Katiba ya nchi na mambo kama hayo, ni yako wewe na Mungu wako. Swali: Kwa hiyo kufa kwa kukosa tiba kwa sababu huna vijisenti ni rasmi? Jibu: Hilo silijui. Halafu nimependekeza kwamba acha ufukuzi wa makaburi. Swali: Nina hoja nyingine; Tanzania, Mozambique, Zambia, Somalia na Sudan ipi imeendelea kuliko nyinginezo? Jibu: Haipo iliyoendelea. Nchi zote ulizozitaja zinasota umasikinini. Kwa mfano, kwetu hapa tunavaa vitu vya mitumba. Nadhani unaelewa. Swali: Hivi kuendelea kwa taifa lolote lile maanake ni nini? Jibu: Taifa likiendelea itabidi uwaulize OWM, au labda na watu kama wa Benki ya Dunia, lakini Benki ya Dunia hawakujui, kwa hiyo acha shughuli hiyo. Swali: Bradha unapenda sana kunikatisha tamaa. Sasa ninakuuliza hivi; hapa nchini tuna magrajueti wangapi? Jibu: Magrajueti? Sijui unawataka wa nini kwa sababu kumbukumbu za namna hiyo ni ngumu kuzipata. Isitoshe hatuna ofisi ya kumbukumbu za aina hiyo. Swali: Unasema hamna, kivije yaani? Jibu: Kwa maan ya kwamba hatuna utaratibu. Kama utaratibu upo basi piga simu OWM watoe agizo ili buku litolewe na wahusika ili watu walinunue na walisome. Swali: Sawa. Kwa hiyo una maana kila aidia mwananchi akiitafuta lazima apige simu OWM? Jibu: Waulize watu wa OWM. Itakubidi kuongea kwa kimombo maana OWM walio wengi wanaongea lugha hiyo. Usije ukajisumbua kivinginevyo. Swali: Mimi kama mimi ninaongea na maofisa wakubwa kuliko wewe. Usinichukulie kama juha bradha. Unanielewa? Jibu: Ninakuelewa. Hata wewe nafikiri unanielewa ndio maana unafokafoka. Swali: Sijafoka bradha. Okay, hapa utanisaidia, ni kiongozi gani katika ngazi ya uwaziri ambaye alikuwa ni hodari kiutendaji? Jibu: Ninavyoelewa hakuna waziri ambaye anaweza kuwa hodari kuliko wengine. Hii ninaongelea kiutendaji yaani. Pamoja na hayo swali lako ni gumu kidogo. Swali: Kwa hiyo, kwa maana hiyo kama ni mkoroganyo ni mkoronganyo tu, sio? Jibu: Bradha mimi sijasemea mikoroganyo. Nimesemea hilo ulilosema uhodari. Kipimo cha uhodari hakipo. Pengine ndio maana, kuharibu na kubabaisha ni vitu ambavyo vipo. Swali: Labda ni mimi ninakukoroga bradha. Tufanye nini ili tuendelee kwa mtazamo wako? Jibu: Punguza blah blah. Barabara ya kutoka Karagwe, Biharamulo, Kasulu, Kibondo, Kigoma, Mpanda, Sumbawanga, Tunduma, Itumba mpaka Malawi ijengwe. Dhahabu zilizopo zitumike. Swali: Sasa ni wewe unaota sio? Jibu: Sijaota wala sioti. Mwana madini mmoja aliyepata ubobezi wa madini Urusi ya siku hizo aliniambia kwamba nchi yetu dongo lake lote limefunika dhahabu. Swali: Halafu ikawaje? Jibu: Pale wizarani alidharauliwa na niliambiwa alihamishiwa makao makuu ya madini. Lakini kama nilivyokueleza hapa na mimi ninachimba kaburi ambalo kuna gogo la mpingo. Swali: Baada ya pale? Jibu: Baada ya pale yule mtaalamu alifariki kivyake lakini alivyonieleza blue print aliyonionyesha haijafa, madhahabu ndiyo kama tunavyoyaona. Swali: Kwa hiyo ni kwamba nchi yetu iko juu ya dhahabu? Jibu: Naam. Swali: Kwa siku hizi kuna injinia yeyote hodari kuhusu mambo haya bila kuzuga? Jibu: Tusimtafute. Kama unatafuta sana jina lake, piga simu OWM. Ushauri wangu. Acha tu. Swali: Kakoloboji e, mimi sifurahii kama unaonyesha kuchoka namna hiyo? Jibu: Mimi naomba tukutane kesho. Naomba niingie daladalani. Gongo la Mboto si Ilala bradha. Ni mbali kidogo. Mpe salamu zangu waifu na binti yako Kifurushi. Simu: 00255762145684 |
No comments:
Post a Comment