Wednesday, February 04, 2009

Jeshi la polisi Norway kuruhusu

wanawake kuvaa hijabu (ushungi)

wakiwa kazini



Keltoum Hasnaoui Missoum (miaka 23) Polisi mwanafunzi


Jeshi la polisi la Norway, litaruhusu polisi wa kike watakaotaka kuvaa hijabu (ushungi) kuvaa vazi hilo. Inspekta Jenerali Mkuu wa polisi, Bi. Ingelin Killengreen amesema sababu ya uamuzi huo, ni kujaribu kutoa nafasi kwa wanawake wenye asili ya kigeni ambao kwa mila na desturi au dini hawawezi kutoka nje bila kuvaa ushungi, kuweza kujiunga na jeshi hilo. 

Dada Keltoum Hasnaoui Missoum (mwenye asili ya Algerie) kutoka mjini wa Sandnes, ambaye ni polisi mwanafunzi, aliandika barua kwa Bi. Ingelin Killengreen kuomba kutumia ushungi akiwa mafunzoni. Hili la polisi wa kike kuruhusiwa kuvaa ushungi wakiwa kazini limezua malumbano makali baina ya wanaopinga na wanaopendelea wazo hilo.

Uamuzi wa mwisho wa suala hilo uko chini ya waziri wa sheria na polisi, Bw. Knut Storberget.




1 comment:

Anonymous said...

hawa ni wanafiki tu, huwezi kutafuta kufanya mambo yako kwenye nchi ya watu,wao kwenye nchi zao hawawezi kukuruhusu kufanya mambo yako kwa uhuru hivyo.