Wednesday, February 04, 2009

Waziri Masha maji shingoni


Waziri wa Mambo ya Ndani na Usalama wa Raia, Lawrence Masha


Waziri wa Mambo ya Ndani na Usalama wa Raia, Lawrence Masha, yuko katika hatihati ya kuendelea na wadhifa huo kutokana na tuhuma inayomkabili ya kuingilia zabuni ya kumtafuta mwekezaji atakayetengeneza vitambulisho vya uraia, hali inayoashiria maji kumfika shingoni.

Kwa mujibu wa taarifa za ndani kutoka bungeni, tayari Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama chini ya Wilson Masilingi, imetangaza kumuweka Masha kitimoto leo (Jumatano) ili kueleza sababu za kuingilia mchakato huo na zaidi kuibeba Kampuni ya Segem Security katika zabuni hiyo, wakati taarifa za kiutendaji zinaonesha kuwa ina historia chafu ya kugawa ‘milungula’ ili kushinda zabuni huko Nigeria.

Taarifa hizo zimedai kwamba, hata kama waziri huyo ataponyoka kwenye kamati hiyo ya Bunge, kuna hatari ya kumalizwa na hoja binafsi inayotazamiwa kuwasilishwa na Mbunge wa Karatu, Wilbroad Peter Slaa (Chadema), ambaye anaonekana kujiridhisha kwa taarifa za kitafiti.

Wakati hali ikiwa hivyo, kuna taarifa za uwepo wa makachero ndani ya Wizara ya Mambo ya Ndani wakichunguza kisa cha kuvuja kwa siri ya mchakato wa zabuni hiyo ikiwa ni pamoja na mtu aliyenyofoa kwenye ‘faili’ barua ya Waziri Masha kwenda kwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kuhusu kashfa hiyo.


Kutoka Global Publishers Limited (TZ)


No comments: