WAZIRI wa Mambo ya Ndani, Lawrence Masha, amesema tuhuma zinazoelekezwa dhidi yake kwamba aliingilia mchakato wa zabuni ya kuchapisha vitambulisho vya taifa ni za kutungwa na hazina ukweli wowote.
Akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano aliouitisha kwa vyombo vichache vya habari, jijini Dar es Salaam, Waziri Masha alisema atakuwa tayari kujiuzulu iwapo itathibitika kuwa aliingilia mchakato huo.
Waziri huyo alisema kuendelea kuwa kimya kuhusu sakata hili, huku tuhuma dhidi yake zikiendelea kumwandama, kunaweza kufanya Watanzania waamini kuwa tuhuma hizo ni za kweli.
Akizungumzia sababu ya yeye kuwa kimya muda wote, alisema ilitokana na kuogopa kuingilia mchakato uliokuwa ukiendelea ndani ya Bunge kuhusu suala hilo ambalo lilikuwa mbele ya Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, baada ya Mbunge wa Karatu, Dk. Wilbrod Slaa, kutaka kuwasilisha hoja binafsi kuhusu jambo hilo...
No comments:
Post a Comment