Wachawi wakutwa
Makongoro Oging’ na Issa Mnally
WANAWAKE wawili wanaosadikiwa ni wachawi, wiki iliyopita walikutwa wakiwanga mchana kweupe katika Mtaa wa Mhonda karibu na Msikiti wa Jamatini uliopo kariakoo jijini Dar es Salaam..
Watu walioshuhudia tukio hili walisema kuwa waliwaona wanawake hao waliovalia nguo za ajabu majira ya Asubuhi, huku wakiwa na kuku jogoo mzima aliyenyonyolewa na kubakizwa manyoya kichwani na katika mkia huku akiwa amefungwa hirizi mguuni na bawani.
Wanawake hao ambao walikaa kimya bila kusema na mtu, walitimua mbio muda mfupi baada ya kumaliza kufanya ushirikina huo ingawa hata hivyo hakuna mtu aliyewafuata kwa kile kilichodaiwa kuwa walikuwa ‘wamejichanja’ dawa inayowafanya watu wakate tamaa ya kuwafuatilia.
Taarifa zaidi zilizopatikana katika eneo la tukio zinadai, kuwa wanawake hao hawakujificha bali walikua barabarani bila uwoga baadaye walimuacha kuku huyo akiduaa, hata hivyo wananchi hasa wafanyabiashara wa maeneo ya Kariakoo walijitokeza kwa wingi kushuhudia tukio hilo la aina yake.
Askari wa Kampuni ya Ulinzi ya Altimate waliokuwa wakilinda Msikiti wa Jamatini siku hiyo, walitimua mbio kwa kuogopa kudhuriwa na tukio hilo la kishirikina lililovuta hisia za watu wengi.
Kila mmoja katika eneo jilo, alikuwa na hisia tofauti kuhusu tukio hilo huku wengi wakionekana kushangaa kuona kuku huyo aliyetobolewa matundu matatu mwilini, akiteseka kwa kupigwa jua kutokana kunyonyolewa manyoya yake karibu yote.
Mmoja wa watu waliohojiwa na Gazeti hili ambaye halikataa kutaja jina lake alisema kuwa, tukio hilo litakuwa limeharibu hali ya biashara mtaani hapo hivyo anahitajika mganga wa kienyeji kulitambikia eneo hilo ndipo mambo yaende sawa.
Hata hivyo, baadhi ya watu walidai kuwa hakuna kitakachotokea hivyo wananchi wasiwe na hofu juu ya hilo, bali waendelee na biashara kama kawaida.
Kijana mmoja ambaye jina lake halikupatikana mara moja, alimchukua kuku huyo na kuondoka naye ingawa haikujulikana alienda naye wapi na kufanya nini.
Tanzania hivi sasa inakabiliwa na vitendo vya kishirikina ambavyo katika siku za hivi karibuni vimewageukia walemavu wa ngozi (maalbino) na vikongwe ambao wamekuwa wakiuawa kikatili hali ambayo imemlazimu Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kufuta kwa muda leseni za waganga wa jadi.

Toka Global Publishers Limited
No comments:
Post a Comment