Monday, February 23, 2009

Waomba ukimbizi

hawatapewa vibali

vya kazi bila

utambulisho wa

kutoka wanakodai

wanatoka





Kuanzia sasa wanaokuja Norway  kuomba hifadhi ya kikimbizi bila ya utambulisho wa wanakodai wanatoka, hawatapewa vibali vya kufanya kazi ya muda huku wakisubiri uamuzi wa kesi zao. Hayo yamesemwa na waziri wa kazi na majumlisho  ya jamii, Bw. Dag Terje Andersen na kunukuliwa na gazeti la VG. Bw. Andersen ameiagiza idara ya wahamiaji (Utlendingsdirektoratet = UDI) kuwa kuanzia sasa wasiwe na mchezo wala huruma kwenye maamuzi ya kesi za wanaokuja bila vitambulisho/pasipoti.

Tisa kati ya kumi ya watu wanaokuja Norway kuomba hifadhi ya kikimbizi hawana aina yoyote ya utambulisho au pasipoti za wanakodai wanatoka, kutokana na takwimu za Idara Kuu ya Takwimu (Statistics Norway)

Mwanzoni wote waliokuwa wanakuja kuomba hifadhi ya kikimbizi walikuwa wanapewa vibali vya kufanya kazi huku wakisubiri uamuzi wa kesi zao.


No comments: