Friday, March 20, 2009


Kasi ya kesi hii ni kazi

kwelikweli



Kwa Waziri wa Mikiki na Makeke,
Uzitoni Street,
Bongo.
 

 

Mpenzi Frank,

Mambo vipi mpenzi wangu?  Bila shaka hujataja neno kondomu tena kwa kuhofia kuzabwa vibao.  Yaani watu!!!  Kama kondomu ni dhambi, shambulio si dhambi pia?  Tena unashambulia watu kwa kunena tu.  Na ingawa jamaa ametiwa ndani kwa kasi ya ajabu, naona wengi bado wanamwunga mkono. 

Lakini mambo mengine vipi?  Maisha yanaendaje?  Utapata safari ya kuja Bongo hivi karibuni maana ninavyokumiss mwisho nitazimia.  Mbona hakuna kondomu ya hisia maana mara nyingine hisia zangu kali zinataka kufurika. 

Upande wangu mimi ni mzima nikijifunza kila siku mambo ya nchi yetu.  Hebu fikiria.  Wanashindwa kulinda hata wanene wa taifa, kisha wanavilaumu vyombo vya habari.  Mimi sijasoma lakini ilibidi nicheke niliposoma hayo. 

Bofya na endelea>>>>>


No comments: