Taifa litaendelea kucheza
Sadakalawe hadi lini?
HIVI tutaendelea kuzungumzia mambo ya ufisadi mpaka lini? Ni jinsi gani kama taifa tutafika mahali na kusema “sasa yatosha”. Je twaweza kuendelea kuzungumzia masuala ya ufisadi kwa miaka nenda miaka rudi bila ya kuchoka na ya kuwa tumeshindwa kutafuta njia ya kuyamaliza yote mara moja na daima? Hizi kesi kubwa za kifisadi tutaendelea nazo mpaka kitokee nini?
Ndugu zangu, nimeanza kujiuliza kama labda tufike mahali tukubali tu yaishe. Tukubali kwamba sisi Watanzania tumejaliwa viongozi goigoi, wagumu kuamua, na wazito kutatua matatizo; kiasi kwamba tuamue tu kuziachilia hizi kesi za kifisadi na tuanza ukurasa mpya.
Kwa kadiri mambo yanavyokwenda, sioni dalili yoyote ya kesi za ufisadi kufikia mwisho kwa mwendo huu ambao tunatumia. Matukio makubwa ya kifisadi ambayo yametingisha nchi na kugusa hisia za wananchi bado yapo na yanaendelea kunguruma, na mengine hata kuanza kushughulikiwa hakuonekani.
No comments:
Post a Comment