


Mambo vipi wapenzi wa shindano hili, ‘Ijumaa Sexiest Girl’, hii hapa ni Ijumaa nyingine bomba ambayo mlikuwa mkiisubiri kwa hamu kubwa ili kufahamu ni nani kati ya Wema Sepetu na Irene Uwoya atafanikiwa kuibuka na ushindi.
Baada ya wiki iliyopita kushikwa na kigugumizi cha kumtaja mshindi ili kuweka mazingira mazuri ikiwemo zawadi, kwa heshima na taadhima na kwa mujibu wa majaji wetu (wasomaji na wapenzi wa shindano hili) leo tunatamka kwaba, mshindi ni Irene Uwoya.
Kwa mujibu wa Mratibu wa shindano hili, Oscar Ndauka, Irene Uwoya amekuwa akiongoza kwa kura nyingi zaidi tangu mpambano huo ulipoanza, ndiyo sababu iliyomfanya leo aibuke na ushindi huo akifuatiwa na Wema Sepetu.
“Baada ya kuibuka na ushindi huo kisha kupewa heshima ya kuwa mrembo mwenye mvuto wa kimapenzi wa gazeti hili, Irene pia atapata fursa ya kufanya ‘shopingi’ ya nguvu ndani ya duka la mavazi ya kisasa, Zizzou Fashions lililopo Sinza, Dar es Salaam kama zawadi.
“Tunawashukuru wote waliyofanikisha shindano hili kukamilika kwa mafanikio, wakiwemo wasomaji na wapenzi wa mpambano huu ambao kwetu sisi ni kama majaji. Pia tunaheshimu mchango wa washiriki wote waliokuwa ndani ya shindano hili tangu mwanzo hadi hii leo ambapo tunamtaja mshindi,” alisema Ndauka.
Kutoka http://abdallahmrisho.blogspot.com/
No comments:
Post a Comment