Ushoga, usagaji ni dhambi
kama dhambi nyinginezo?
TOLEO lililopita nilijadili juu ya ubikira wa Bikira Maria. Mada hiyo imezua maswali mengi. Nilipata sms nyingi na barua pepe. Kubwa lililojitokeza ni kwamba majadiliano ni muhimu hasa kwa mambo ambayo yanaonekana kuwa na utata na yanagusa maisha ya watu wengi katika jamii yetu.
Baadhi waliniomba nianzishe mjadala juu ya ushoga na usagaji. Nimekubali kufanya hivyo kwa uangalifu mkubwa; vinginevyo kuna hatari ya kuzabwa vibao kama ilivyomtokea mzee Mwinyi.
Oktoba mosi, 1986 Kadinali Ratzinger (sasa ni Papa Benedict wa 16), alitoa mwongozo wa Kanisa Katoliki juu ya watu wanaovutiwa na jinsia zao (homosexuality).
Mwogozo huu ilikuwa ni barua aliyowaandikia maaskofu wote wa Kanisa Katoliki - “On the pastoral care of homosexuals”. Katika barua hiyo, Kadinali Ratzinger aliwakumbusha maaskofu juu ya mwongozo mwingine kuhusu suala hili hili uliotolewa Desemba 1975 - “Declaration of Certain Questions Concerning Sexual Ethics” uliosisitiza kwamba hali ya mtu kuvutiwa na jinsia yake ifanyiwe utafiti na ichukuliwe kwa uangalifu na busara.
1 comment:
Padri,
Umenena!
Post a Comment