Mtoto mmoja mdogo alikuwa akiongea na baba yake kuhusu suala la kuoa na mazungumzo kati ya wawili hao yalikuwa kama ifuatavyo:
Mtoto: Baba mimi nataka kuoa!
Baba: Mh! Unataka kumuoa nani?
Mtoto: Nataka kumuoa bibi
Baba: We mtoto, yaani unataka kumuoa mama yangu, haiwezekani na hata mila na desturi zetu haziruhusu
Mtoto: Kama haiwezekani mimi kumuoa mama yako mbona wewe umemuoa mama yangu?
Baba akabaki hana jibu...
Kutoka Global Publishers TZ
No comments:
Post a Comment