Thursday, March 19, 2009

Atapeliwa

Kroner milioni 1,7 

na ”Wanaijeria”

 

kwa barua ya

urithi!!!




Mama mmoja wa Kinorwejiani ametapeliwa Kroner milioni moja na laki saba (1,7 milioni kroner). Mama huyo amezitoa hizo hela, baada ya kupokea barua kuwa akitoa hizo hela atapata sehemu ya urithi wa huyo mwandishi wa hiyo barua wa Kroner milioni thelathini na mbili (32 milioni). Hayo yamethibitishwa na mshauri wa kitengo cha polisi kinachoshughulikia utapeli, uhalifu wa kiuchumi, wizi wa mali za umma na uhujumu wa mazingira (ØKOKRIM), Bi. Anne Dybo. Bi. Dybo ameliambia gazeti la Adresseavisen.


Bofya na angalia kuhusu hili la hizi barua za ”Kinaijeria”


1 comment:

Anonymous said...

Wajinga ndio wakiwao! Mpaka leo hii kuna watu bado wanatapeliwa na huu wizi? Waache watapaliwe. Huyu mama hasomi magazeti au kuangalia TV? Hata redio basi?