Thursday, April 09, 2009


Anguko la Uchumi:

Tatizo wazalendo

ni hohehahe




na Dk. Haji Hatibu Haji Semboja

MTIKISIKO wa soko la kifedha unatofautiana kufuatana na kiwango cha maendeleo, taasisi, nchi na nchi na ni matokeo ya sababu nyingi za misambaratiko.

Kiwango cha mwanzo na cha chini ni cha jamii, (micro level). Mtikitiso wa kifedha unatokana na sababu mbalimbali hususan katika tabia, maamuzi na mwenendo wa jamii katika masoko ya nyumba na mikopo ya ujenzi. Ni vema kusema kuwa sera za kuhuisha wingi na viwango vya huduma za makazi, nyumba bora za jamii, ni moja ya mambo mengi muhimu katika kuleta maendeleo ya kijamii na kiuchumi wa taifa.

Watu, taasisi, serikali na jamii zote zinapenda kuwa na vitu na maisha bora kwa wote. Hata hivyo, katika kufikia malengo na madhumuni hayo, si vema sheria na taratibu za uendeshaji wa taasisi za kifedha kuvunjwa. Watu, taasisi za kifedha na za serikali zimekuwa si makini katika kuhakikisha kuwa jamii inapata na kufuata sheria na taraatibu za ujenzi wa majumba, nyumba na miundombinu kwa kutumia mikopo kutoka katika taasisi za kifedha

…bofya na endelea>>>>


No comments: