
Kwa nini mtu maarufu akiuke
taratibu na sheria,
awe mwanasiasa,
awe mwanamuziki?
Kwa Waziri wa Mikiki na Makeke,
Uzitoni Street,
Bongo.
Mpenzi Frank,
U hali gani huko? Mvua inanyesha kweli au ni kama ahadi za wanasiasa hapa? Maana ahadi ni nyingi lakini utekelezaji sifuri. Hapa mawingu ni ahadi lakini mvua ndiyo hivyo tena. Matokeo yake ni joto, joto, joto.
Jasho tupu bila mafanikio. Hata bosi analalamika ingawa nadhani anakaa kwenye joto kama dakika kumi tu kwa siku ... yaani akitoka mlangoni mwa nyumba hadi kufikia mlango wa gari na kutoka mlango wa gari hadi mlango wa ofisi, na kurudi tena jioni. Kwa hilo anahitaji leso tatu!
Chumbani mwangu ndiyo hivyo tena, maana viyoyozi vinayoyoma kabla ya kufika kwa Hidaya. Kwa sababu ya kazi, angalau nachelewa kulala kisha naoga na kujitupa kitandani bila hata kujikausha. Vinginevyo, wangedhani nimekuwa kikojozi
No comments:
Post a Comment