Baada Uroa kuwekewa
Umeme, wakazi wake
wapunguza kufanya
ngono!!!
Mwanaathropojia wa jamii na mhandisi, Bi. Tanja Winther amethibitisha kwenye utafiti wake alioufanya kwenye kijiji cha Uroa Mashariki ya Unguja (Zanzibar). Bi. Tanja amekaa Uroa muda mrefu kwa ajili ya utafiti huo. Kwenye utafiti huo, inaonyesha kuwa wasichana wengi wamepata nafasi ya kuhudhuria shule kwa sababu kumewekwa mabomba ya maji kijiji hapo. Pia wake kwa waume wamepunguza ngono baada ya kuwekwa umeme kwenye kijiji hicho. Bi, Tanja anaandika kuwa wake kwa waume, wanatumia muda mrefu usiku kuangalia runinga (luninga), hivyo inapofika wakati wa kulala wamekuwa wamechoka hoi bin taabani, hivyo kusababisha upungufu wa shughuli za “tendo la ndoa”. Bi. Tanja Winther yuko Chuo Kikuu cha Oslo.
Kitabu chake kinaitwa “THE IMPACT OF ELECTRICITY Development, Desires and Dilemmas” kimechapwa na Berhahn Books. Kitabu hicho pia kimetafsiriwa kwa Kiswahili.
No comments:
Post a Comment