Saturday, April 25, 2009


Virusi vya bombo

la kutisha vyaingia

Norway


Wanorwejiani wanaotoka likizo nchi za Mexico na Kusini ya Marekani, wamekuwa wakirudi na virusi vya bombo (influenza) vya aina ya A/H1N1 ambavyo ni hatari kwa maisha ya binadamu. Hadi hivi sasa virusi hivyo vimeshaua watu 68 nchini Mexico, na wengine 8 wako taabani bin mahututi nchini Marekani, idara ya afya nchini Norway, ”Folkehelseintituttet” imeonya. 

Mpaka sasa hakujarepotiwa kuumwa kwa mtu yeyote Ulaya au hapa Norway.  Shirika la afya duniani, WHO linahofia kuwa virusi hivyo vinaweza kusababisha kufa kwa halaiki ya watu duniani, imeripoti CNN.

No comments: