
Makosa 10 wanawake wengi
huyafanya bila kujijua
Naomba kwanza nimshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunipa nafasi hii tena ya kuweza kuchangia hapa leo. Nawashukuru na ninyi ndugu zangu mnaondelea kuniandikia, inanifariji mno kupata kusikia kutoka kwenu. Na inanipa nguvu yakuendelea…
Mzigo ndiyo huu uko hewani namna hii, sisi huku tunakula bata mida hii wenzenu, (kwa wale wenzangu na mimi kula bata ni kufurahia maisha, au unaweza kusema kustarehe kwa lugha nyepesi...) Naomba niwakumbushe jamani, tunaishi mara moja tuuu. Make the most of it…Msiache kufurahia hizi siku za maisha, unajua kuna sababu kwanini mko hai hadi leo.... ushanifaham. Na hiyo basi inanileta moja kwa moja katika hoja yangu hii leo; Kufurahia maisha…!Naomba niwachukue niwapeleke "behind the scenes" kule wanawake wengi wanakoungumia.
Kuna kesi nyingi nimezisikia, na nyingine nimezisoma na kuziskia kwenye vyombo mbalimbali vya habari; 'Mwanamke ajiua' 'Mwanamke ajiua na kuangamiza familia yake'
Inasikitisha…! Lakini hili si lakuacha lipite…
Wataalam wa mambo ya akili wamegundua kuwa mlimbikizo wa mawazo (Stress) unaeweza kupelekea ugonjwa huu wa akili ambao humfanya mwanamke kuhisi hana thamani na suluhisho ni kuamua kusitisha maisha yake na wakati mwingine ya wale waliokaribu naye.
Kitu ambacho wanawake wengi hawatambui ni kwamba hali hii inaweza kutokea endapo utaruhusu maumivu ya moyo yatawale akili yako. Wanawake tumeumbwa na nguvu ambayo kama tutaitumia Ipasavyo, tutaishi tupendavyo… mmenisoma?
Na leo nataka kuliongela hili kwa kina. Kutoruhusu matatizo yatawale akili yako. .
Kuna makosa 10 wanawake wengi huyafanya bila kujua haya ni yakuepuka na leo niko hapa kuyachambua:-
1) USIAMINI KUPITILIZA
Ukijipa mia kwa mia kuwa hutokaa utendwe jua uko katika nafasi kubwa ya kuja kuumia kupitiliza pale utakapokuja kugundua kuwa uliyemuamini kupitiliza siye. Jenga imani kuwa kila kitu kinawezekana… kisha omba Mungu atasaidia, na hata likikufika basi umejiandaa.
2) USIWE TEGEMEZI
Unapokuwa tegemizi mara nyingi ndiye ambaye utakuja kuumia zaidi pale mambo yanapokuja kukugeukia. Kujishughulisha nako kunasaidia kupoteza mawazo kiasi fulani. Na ukweli ni kwamba kusubiri uletewe ndiko ambako kunaleta mitafaruku katika uhusiano na kupelekea kuchokwa.
3) JIFUNZE KUPIGA MOYO KONDE
Hakuna njia nzuri ya kuyakabili matatizo ya nyumba kama kukubali na kupiga moyo konde. Kujishusha na kuomba msamaha ikibidi. Inaweza kuwa kazi ngumu lakini ni njia nzuri ya kukuepushia maumivu zaidi natayoweza kukuondoea msongamano wa mawazo.
4) USIJILAUMU
Usikubali hata siku moja kujiuguza kwa maumivu ya lawama unayojipa. Jua kuwa katika kila wakati mgumu kuna kheri mbele yake. Subira ni ngumu lakini muhumu sana katika maisha ya mwanamke.
5) JIPENDE MWENYEWE KWANZA
Unapoamua kuweka mbele mtu mwingine zaidi yako unakuwa hujitendei haki. Mwengine anaweza kukusaliti lakini wewe huwezi kujisaliti. Ukijifunza kujipenda mwenyewe kwanza hutokonda wala kuruhusu kuumia na vitu vidogo vidogo.
6) USILIMBIKIZE MAWAZO…
Wanawake wengi wanadiriki kufa na vitu kifuani mwao, jua kwamba wakati mwingine huwezi kufanya kila kitu wewe kama wewe. Tafuta msaada kwa watu wazima, uondokane na huo mzigo kifuani mwako.
7) USIJIUMIZE BILA SABABU
Unaposhindwa kufanya vitu vya maana kwa kukaa hapo kufikiria tabu za maisha yako wakati mwingine unapoteza muda wa bure. Fanya kitu tofauti na mazoea inawezakukusaidia kuona ulimwengu mwingine ambao huenda ulikuwa huujui.
8) USIFICHE MAUMIVU
Usijaribu hata siku moja kuficha maumivu wakati unaumia, tafuta njia ya kutatua matatizo yako once and for all.
9) USIJISUMBUE KUMBADILI MUME
Nilishawahi kusema kuwa hakuna mwenye uwezo wa kumbadili mtu mwingine, isipokuwa mtu mwenyewe akubali kubadilika. Sasa badala ya kuungumia na namna ya kumbadili ni vyema ukakubali matokeo.
10) JITAMBUE
Ni muhimu kwa kila mwanamke kutambua na kuelewa kuwa yeye ni kiumbe muhimu katika jamii. Yeye ndiye muongozo wa kizazi kijacho. Yeye ndiye tumaini. Kwa kutoruhusu matatizo yatawale akili yako, utasevu maisha yako na ya wale wanaokutegemea.
Pole na karibu tuwe sote tena hapa wiki ijayo:
- asmahmakau@mwananchi.co.tz
No comments:
Post a Comment