Monday, April 13, 2009

Mtangazaji wa Habari

Aliyejipaka Rangi Nyeusi

Kujifananisha na

Obama Azua Balaa




Mtangazaji huyo wa luninga alitangaza taarifa ya habari huku akiwa amejipaka rangi nyeusi uso wake katika kumuigizia rais Obama ambaye alikuwa nchini humo kwenye ziara yake ya siku mbili katika ziara yake ya siku nane barani Ulaya.

Pamoja na kwamba haikujulikana wazi kama mtangazaji huyo alikuwa na nia ya kuleta ubaguzi wa rangi au la, video yake hiyo imezua hasira kwa wengi walioiona ni ya kibaguzi.

Vyanzo vya habari vya Uturuki vilijaribu kuuficha mkasa wa video hiyo na kudai kwamba video hiyo ililenga kumpa kidongo rais wa zamani wa Marekani George Bush ambaye walisema aliutia gizani uso wa Waturuki na kudai kwamba uigizaji wa mtangazaji huyo wa habari ulilenga kuonyesha matumaini yao kwa Obama kwamba atabadilisha hali iliyokuwepo.

Kwa tafsiri ya haraka haraka mtangazaji huyo alisikika kwenye taarifa ya habari hiyo akisema " Bwana Obama, umeiteka mioyo yetu na ukarimu wako, tutafanya yote Marekani itakayotaka tufanye kama rafiki zake, lakini sasa tunataka na nyie mfanye kama sisi".

Website nyingi za Marekani kama vile Rightpundits.com zimelaani ubaguzi wa rangi aliofanyiwa rais wa Marekani na kumuuita mtangazaji huyo kuwa ni "Mbaguzi wa rangi mpumbavu".


Kutoka: www.nifahamishe.com 


No comments: