Thursday, April 30, 2009

Vunja mbavu


Mchaga na dili la pesa

Jamaa mmoja wa kichaga alikuwa anasumbuliwa na uvimbe tumboni. Ndugu zake wakaamua kumpeleka hospitali, akatakiwa afanyiwe operesheni. Gharama za Matibabu zilitakiwa milioni mbili.Ndugu na jamaa wakahangishana wakapata pesa hizo kisha wakampatia Dokta ili amfanyie upasuaji ndugu yao. Ile ndugu wanaondoka tu hospitalini pale, mazungumzo kati ya mgonjwa na daktari yakawa hivi: 

Mgonjwa: Dokta nataka tufanye dili la pesa. Mimi naona huu uvimbe achana nao, nishone tu ili wakija wajue umenifanyia operesheni. Kwenye hizo milioni mbili chukua laki tano niachie moja na nusu , nipate za kunywea bia! Msingi wa biashara hawataki kunipatia ila pesa ya kunitibia wanatoa, huu si ujinga Dokta. 

Dokta akabaki ameduwaa...

Kutoka Global Publishers

No comments: