
Wamesahau kwamba hata
wakivaa masuti ya namna gani,
bado watanuka tu
Kwa Waziri wa Mikiki na Makeke,
Uzitoni Street,
Bongo.
Mpenzi Frank,
KWANZA asante sana kwa marashi uliyoniletea. Jamani! Nilipoweka kidogo, hata mama bosi akaanza kunionea gele. Nakupenda mpenzi unavyonipenda.
Na baada ya hapo, mambo vipi huko jamani? Wazima au wazimu? Maana mambo ya Bongo letu yanatia wazimu tu. Hujui nani wa kumzimia na nani wa kumzamia.
Ukiona huyu kweli ni mfano mzuri, kesho ameshakashifiwa na mwenzie. Kisha hujui umwamini nani na usimwamini nani maana inaonekana lengo la wote hao ni kuchafuliana jina, ungedhani maadui tangu enzi na enzi.
Ndiyo maana pia nashindwa kuwaelewa hawa wa chama cha wanene ambao wanapenda kuwatisha watu nje ya chama chao eti wanasema ni mafisadi.
No comments:
Post a Comment