Waziri Kiongozi awasha moto

na Mwanne Mashugu, Zanzibar.
WAZIRI Kiongozi, Shamsi Vuai Nahodha, ametoa kauli nzito ndani ya Baraza la Wawakilishi kuwa, hakuridhishwa na mjadala wa mafuta na gesi asilia kuondolewa katika orodha ya mambo ya Muungano.
Waziri Kiongozi ametoa kauli hiyo siku chache tangu yeye binafsi kushutumiwa kutohudhuria kikao cha kwanza cha mjadala huo, na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Rais (Muungano), Mohammed Seif Khatib, akielezwa na wajumbe wa baraza hilo kuwa ni msaliti wa Wazanzibari. Akichangia waraka wa serikali kuhusu utafiti na uchimbaji wa mafuta na gesi asilia, Waziri Kiongozi alisema baadhi ya wajumbe, walivuka mipaka na hoja zao kutawaliwa na jazba kitendo ambacho kinakwenda kinyume na kanuni za Baraza hilo.
Alisema mjadala ulikuwa mzuri, lakini ulitawaliwa na kasoro hiyo, kitendo ambacho alikikemea kwa vile wajumbe wa Baraza watakapoanza kudharauliana ndani ya Baraza na wao watadharauliwa zaidi wawapo nje Baraza hilo…
No comments:
Post a Comment