Anusurika kufa baada
ya kuchomwa
kisu na bwana´ke
wa zamani.
Polisi walifika mahali pa tukio, dakika chache tu baada ya kuarifiwa.
Mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka thelathini alinusurika kufa jana, baadaya ya kuchomwa kisu mara kadhaa sehemu ya mgongoni na mapajani na bwana wake wa zamani. Tukio hilo lilitokea jana jioni kwenye bustani ya Sofienberg, mjini Oslo. Jamaa amewekwa lupango na atapelekwa mahakamani siku ya Jumatatu. Huyo mwanamke alikuwa na mtoto wake (polisi wamekataa kutaja umri wa huyo mtoto), walikuwa njiani kutoka kwenye bustani kwenda kwenye gari yake, ndipo jamaa alipomshambulia.
No comments:
Post a Comment