Friday, May 01, 2009




Kutoka Alasiri

Milipuko ya mabomu, makombora na risasi ambayo ilitikisa Jiji la Dar es Salaam jana imeendelea kuzusha kihoro, huku idadi ya watu waliokufa na wale waliojeruhiwa kutokana na tukio hilo ikizidi kuongezeka. ..bofya na endelea>>>>>

 

Kutoka Global Publishers

Majonzi, vilio na hali ya mashaka, bado inatawala sehemu kubwa ya wakazi wa Jiji la Dar es Salaam hususan wale wanaoishi wilayani Temeke, kufuatia matokeo ya milipuko ya mabomu juzi kwenye kambi ya Jeshi, Mbagala Kizuiani.Jana, baadhi ya watu walisitisha shughuli zao za kibiashara au kuomba ruhusa makazini, wengine wakitumia nafasi hiyo kuwatafuta wapendwa wao waliopotezana baada ya milipuko na baadhi wakilitulia kwa hofu...bofya na endelea>>>>>

 

Kutoka Nipashe

Idadi ya watu waliokufa kutokana na milipuko ya mabomu katika ghala la kuhifadhi silaha la Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) katika Kambi ya Mbagala, jijini Dar es Salaam, imeongezeka kutoka watatu hadi 13, kati yao inahofiwa kuwa watano ni wanajeshi. ..bofya na endelea>>>>>

 

Kutoka Habari Leo

Watu 11 wakiwamo wanajeshi sita, wamethibitika kufa katika milipuko ya makombora na mabomu iliyotokea juzi katika kambi ya maghala ya silaha ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Mbagala Kizuiani, Dar es Salaam. Idadi hiyo ya vifo imeongezeka ikilinganishwa na ya juzi, ambapo ilithibitika kuwa watu watatu walikufa katika milipuko hiyo wote wakiwa raia, akiwamo mwanamke mkazi wa Mbagala Kuu eneo la Mwanamtoti aliyekatwa kiuno na chuma cha makombora…bofya na endelea>>>>>

 

Kutoka Majira

IDADI ya watu waliopoteza maisha katika milipuko ya mabomu juzi katika kambi ya ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) iliyopo eneo la Mbagala Kizuiani Dar es Salaam, imeongezeka kutoka  watatu na kufikia saba. Wakati idadi ya watu waliothibitishwa kufa  ikiwa imeongeza, idadi ya majeruhi imeanza kupungua kutokana na wengi  kuruhusu baada ya kupatiwa matibabu…bofya na endelea>>>>>

 

Kutoka Mwananchi

TAARIFA muhimu inayohusiana na tukio na madhara halisi yaliyosababishwa na mlipuko wa mabomu katika kambi ya Jeshi la Wananchi (JWTZ), itakabidhiwa kwa Rais Jakaya Kikwete na Mkuu wa Majeshi, Jenerali Davis Mwamunyange hivi karibuni…bofya na endelea>>>>>

 

Kutoka Uhuru

RAIS Jakaya Kikwete ametembelea kambi ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Mbagala, Dar es Salaam kushuhudia hali halisi katika maeneo yalikotokea milipuko ya makombora juzi. Rais, ambaye ni Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, pia alitembelea hospitali za Temeke na Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI), kuwafariji wananchi waliolazwa kutokana na kujeruhiwa katika tukio hilo…bofya na endelea>>>>>


No comments: