Monday, May 04, 2009

Mengi vs. Rostam


Kutoka Habari Leo

Mfanyabiashara bunge wa Igunga, Rostam Aziz, amemuelezea Mwenyekiti Mtendaji wa IPP, Reginald Mengi kuwa ni nyangumi wa ufisadi na akatangaza kupeleka faili lenye ushahidi wa matendo yake maovu kwa vyombo husika ili vimchunguze…bofya na soma zaidi>>>>>

 

Kutoka Majira

MBUNGE wa Jimbo la Igunga mkoani Tabora, Bw. Rostam Azizi (CCM), ameibuka na kukanusha  madai ya ufisadi dhidi yake yalitolewa hivi karibuni na mfanyanishara mmoja maarufu nchini, huku akieleza kuwa hayana msingi .Bw. Rostam alisema tuhuma zimemvunjia heshima kwa kiasi kikubwa ndani ya jamii kutokana na nafasi yake kama kiongozi wa kuchaguliwa na wananchi katika nyadhifa mbalimbali…bofya na soma zaidi>>>>>

 

Kutoka Mtanzania

MBUNGE wa Igunga, Rostam Aziz, ameinuka na kujibu shutuma nzito zilizotolewa na Mwenyekiti wa IPP, Reginald Mengi, kuwa yeye na watu wengine wanne ni ‘mafisadi papa’, akisema Mengi ndiye ‘fisadi nyangumi’…bofya na soma zaidi>>>>> 

 

Kutoka Mwananchi

MFANYABIASHARA wa jijini Dar es salaam, Reginald Mengi aliwabatiza wafayabiashara wenzake watano jina la "mapapa wa ufisadi", na sasa mmoja wa waliotuhumiwa amejibu mapigo kwa kumbatiza jina la "nyangumi wa ufisadi"…bofya na soma zaidi>>>>>

 

Kutoka Tanzania Daima

VITA ya maneno inayohusisha mapambano dhidi ya ufisadi aliyoianzisha Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Reginald Mengi wiki iliyopita, sasa imeanza kuibua masuala mapya. Katika hali ambayo haikutarajiwa, mmoja wa wafanyabiashara watano ambao aliwatuhumu kwa kile alichokiita ufisadi papa, jana aliibuka hadharani na kutoa tuhuma nzito dhidi yake, akimhusisha na vitendo mbalimbali vya ufisadi alivyodai vimechangia katika kuwafanya Watanzania kuwa maskini zaidi…bofya na soma zaidi>>>>>

No comments: