Samantha Orobator yuko kwenye hatari za kuuawa kwa kupigwa risasi akikutwa na hatia kwenye kesi inayomkabili ya kukamatwa na midaharati. Alikamatwa Agosti mwaka jana kwenye uwanja wa ndege wa Wattay, mjini Vientiane, Laos. Samantha alikamatwa na gram 680 za madawa ya kulevya kufuatia na taarifa za mwendesha mashtaka wa serikali ya Laos. Mwenye kukamatwa na madawa ya kulevya yanayozidi gram 500, hukumu yake ni kifo kwenye sheria za makosa ya jinai za Laos.
Taarifa za kikundi cha kutetea haki za binadamu, kinachomtetea Reprieve, zinasema kuwa Samantha hajakutana na wakili tangu akamatwe mwaka jana. Samantha ni mja mzito miezi mitano. Inasadikiwa kuwa alibakwa akiwa jela.
Ubalozi wa Uingereza nchini Thailand, ulipata taarifa za kukamatwa kwa Sam miezi kadhaa, baada ya Samantha kukamatwa. Uingereza haina ofisi ya ubalozi nchini Laos. Inategemea ofisi yake iliyoko Bangkok nchini Thailand. Ofisa toka ofisi ya Uingereza nchini Thailand, anaruhusiwa kumwona Sam, dakika 20 tu, mara moja kila mwezi.
Sam alikuwa likizoni Uholanzi, Thailand na Laos. Alizaliwa Naijeria, na amekulia kusini ya London.
No comments:
Post a Comment