Rais Obama na msaidizi wake walikuwa wakapate "lanchi" ikulu lakini Obama na makamu wake Joe Biden waliamua kwenda kwenye mgahawa mmoja mdogo wa kawaida tu unaoitwa Ray’s Hell Burgers.
Pamoja na viongozi hao wakuu wa Marekani kuwa miongoni mwa wateja, sheria za kupanga foleni zilifuatwa kama kawaida kwa Obama na makamu wake kupanga foleni nyuma ya wateja waliokuwa wamewatangulia kufika.
Baada ya kuagizia chakula chao Rais Obama na makamu wake walisiti kwenye kona moja wakisubiria kwa hamu chakula chao kiwe tayari.
Rais Obama alilipia chakula chake na kumlipia makamu wake Joe Biden chakula chake na baadae kuwaachia chenji ya dola tano wahudumu wa mgahawa huo.
Watu waliokuwemo kwenye mgahawa huo walipata fursa ya kupiga stori na kupiga picha na rais Obama na makamu wake.
Watu wengine walijazana nje ya mgahawa baada ya polisi kuweka mpaka wa kuzuia wateja zaidi kuingia kwenye mgahawa huo wakati rais Obama alipokuwa ndani.
Kila mtu alikuwa akijaribu kupata kumbukumbu ya tukio hilo kwa kujaribu kupiga picha kwa kutumia kamera za simu zao.
No comments:
Post a Comment