Refarii aitoa
Chelsea kwenye
nusu fainali.
Chelsea 1 – Barcelona 1
Barcelona fainali
kwa ushindi wa goli la ugenini.
Chelsea ndo´walikuwa wa kwanza kufunga goli kwenye dakika ya 9 ya mchezo, kwa goli lililofungwa na Michael Essien kwa kombora toka kama mita 30 hivi. Kipa wa Barcelona, Victor Valdes hakuona kitu. Chelsea waliwabana Barcelona kwa ukuta wa Berlin! Barcelona walikuwa wakishambulia, lakini hawakuweza kupenya ukuta wa wa The Blue (Chelsea) na hata hawakupata nafasi ya kupiga mashuti kwenye goli la Chelsea.
Refarii alianza kuchemsha kuchezesha pale Malouda wa Chelsea alipoangushwa ndani ya mita 16. Hii ilikuwa penalti ya wazi. Penalti ingine aliyoifumbia macho, ni pale Didier Drogba alipoangushwa na Eric Abidal ndani ya mita 16 kwenye goli la Barcelona. Badala yake, refarii akampa kadi nyekundu Abidal kwa kumwangusha Drogba (Chelsea) ndani ya mita 16 kwenye goli la Barcelona. Ilikuwa dakika ya 20 ya tangu kipindi cha pili kuanza. Hapa pia refarii alichemsha. Kosa alilofanya Abidal, halikuwa la kupewa kadi nyekundu.
Barcelona wakicheza ndani na wachezaji tisa, walisawazisha goli kwenye dakika ya 93 lililofungwa na Andres Iniesta. Dakika ya 94, Eto´o alizuia kwa mkono ndani ya mita 16, mkwaju iliopigwa na Michael Ballack. Refarii alikuwa mita 5 tu mbele ya Eto´o, akamezea kupiga filimbi ya penalti. Wachezaji wa Chelsea wakachemka!
Chelsea wakijiona wana damu ya kunguni, wamekasirishwa na uamuzi wa refarii (ambaye pia ni mwanasaikolojia) Mnorwejiani Tom Henning Øvrebø, kwa kuwanyima penalti karibu tatu za wazi kabisa. Drogba aliingia uwanjani na hasira kwa kumsemesha refarii, ilibidi ashikwe na walinzi. Drogba aliendelea kuloloma mbele ya kamera ya luninga kwa kusema kuwa uamuzi wa refa, Tom Henning Øvrebø ni aibu kwa mchezo wa soka.
No comments:
Post a Comment