Thursday, May 07, 2009

Vunja mbavu


Kichaa anapomuokoa mwezake bwawani


Daktari mkuu alimuita kichaa mmoja aliyemuokoa mwenzake kwenye bwawa la kuogelea. Haya yalikuwa mazungumzo yao:

Daktari: Nakupongeza kwa kumuokoa mwenzako asizame na kufa maji.

Kichaa: Usijali yule ni rafiki yangu

Daktari: Kwa sababu hiyo nakuruhusu urudi nyumbani ila nina habari mbaya kwako ni kwamba mwenzako uliyemuokoa amejiua kwa kujinyonga kwenye kamba ya kuanikia nguo.

Kichaa: Hapana, hakujinyonga ila nilimuanika mimi akauke baada ya kuloa...

Kutoka Global Publishers

No comments: