Saturday, May 02, 2009

Wafanya ngono mchana

kweupe mbele ya Hekalu

la Malkia wa Uingereza



Ilikuwa ni mchana kweupe wakati Malkia Elizabeth II wa Uingereza akiwa ndani ya jumba lake la kifahari la Windsor Castle, walinzi wanaomlinda walikuwa wanatimiza wajibu kama kawaida, watalii toka nchi mbali mbali duniani walikuwa wamejazana mbele ya jengo hilo wakitalii.

Hali ilikuwa tofauti pale wapenzi wawili Joy Taylor na Phil Carden walipowasili eneo hilo kutoka kwenye baa ya jirani na kusaula nguo zote na kuanza kufanya mapenzi kweupe kwenye majani yaliyopo kwenye bustani iliyopo mbele ya jengo hilo.

"Dirisha moja katika chumba cha walinzi wa jengo hilo lilifunguliwa na mmoja wa walinzi hao alipoona kinachoendelea aliwaambia wenzake na matokeo yake madirisha mengi kwenye jengo hilo yalifunguliwa na watu wakawa wanachungulia" alisema shuhuda mmoja wa tukio hilo alipokuwa akiongea na gazeti la The Sun la Uingereza.

"Wapenzi hao hawakujali nani alikuwa akiwaangalia, waliendelea kufanya mapenzi kwenye majani kama vile wako chumbani kwao" alisema shuhuda mwingine.

Watalii wa Kijapan waliwachukua video wapenzi hao ambao hawakujali na kuendelea na shughuli yao mpaka pale maafisa wa polisi walipofika eneo hilo.

Polisi wa Uingereza walisema kwamba wapenzi hao walipewa barua ya onyo kwa kukiuka maadili katika sehemu yenye mkusanyiko wa watu.

Malkia Elizabeth alikuwa ndani ya jengo hilo wakati wa tukio lakini ofisi yake ilikataa kusema chochote.

No comments: