Friday, June 05, 2009

Abambwa

kwenye Facebook.

Afungwa miezi sita!



Mwanamke mmoja amehukumiwa kifungo cha miezi sita, baada ya kugunduliwa kwenye Facebook kuwa anakaa na hawara na alidanganya kuwa anakaa pekee na watoto huku akila hela za ustawi wa jamii.

Mwanamke huyo mwenye watoto wawili, amekuwa akilipwa na ustawi wa jamii hela za kutunza watoto na za kuweza kumudu maisha kuanzia 1. Agosti 2003 hadi Januari 2006. Hadi alipokamatwa, alikuwa tayari ameshalipwa Kroner 350 000 (lakini tatu na hamsini elfu) kama T.shs. 74.900.000/= (milioni sabini na nne na laki tisa).

Kwenye fomu za maombi ya kusaidiwa za ustawi wa jamii, mwanamke huyo aliandika kuwa ana watoto wawili na hana mume. Idara ya uchunguzi ya ustawi wa jamii Norway (NAV) ya mkoa wa Buskerud katika kuvinjari kwenye Facebook baada ya ya kutonywa na watu, wakaona jina kamili la huyo mwanamke na maelezo binafsi yake ameandika kuwa anakaa na hawara. Mwanamama huyo akabanwa na NAV – Buskerud na akaweka karata zote mezani kukubali kuwa ameshindwa na kweli alidanganya.

Funzo: Hizi jamii mtandao si za kuandika kila kitu. Ukiandika kila kitu, hakikisha huna rekodi mbaya!!! 

No comments: