Rais Mstahafu Ben Mkapa kwenye mkutano wa

Mhariri wa CCW Oslo, Sarpsborg, Norway
Rais Mstahafu wa awamu ya tatu, Benjamin William Mkapa, yupo Norway kwenye mkutano wa CC9 kuhusu mabadiliko ya mazingira duniani. Mkutano huo ulioanza jana kwenye ukumbi wa Hafslund Manor kwenye mjini wa Sarpsborg, unamalizika leo na kesho kutakuwa na tamasha la watoto. Mkutano huo ulifunguliwa na Mfalme Mtarajiwa, Haakon akiwa pamoja na Malkia mtarajiwa, Mette-Marit. Miongoni mwa washiriki wa mkutano huu ni: Wakili Robert F. Kennedy (mpwa wa John F. Kennedy); Waziri Mkuu wa Norway, Jens Stoltenberg; José María Figueres, Rais mstahafu wa Costa Rica; Jennifer Shipley, Waziri Mkuu mstahafu wa New Zealand; Benjamin Mkapa, Rais Mstahafu wa Tanzania na waziri wa mambo za nje wa Niger, Aïchatou Mindaoudou. Mkutano huu ni wa matayarisho ya mkutano mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu mabadiliko ya mazingira, utakaofanyika Copenhagen, Denmark – Desemba mwaka huu. Mkutano huu umedhaminiwa na kampuni ya nishati ya Hafslund na asasi isiyo ya kiserikali inayotetea mazingira ya Bellona.
Kwenye tamasha la watoto kesho, kutakuwepo mshindi wa Euro Song Contest 2009, Alexander Rybak.
No comments:
Post a Comment