Siku tano kabla ya Air France AF 447 Airbus 300 – 200 kupotea kwenye bahari ya Atlantiki, shirika la ndege la Air France lilipigiwa simu ya tishio la bomu, Jumatano 27. Mei kabla ndege moja ya Air France kupaa toka uwanja wa ndege wa Ezeiza mjini Buenos Aires- Argentina kuelekea Charles de Gaulle mjini Paris. Uwanja huo ulifungwa kwa muda, wazima moto, polisi na wanausalama wa uwanja huo, waliikagua ndege hiyo nje na ndani, kwa mapana na marefu na hawakuona kitu. Baada ya nusu saa, ndege hiyo iliruhusiwa kuondoka Buenos Aires kuelekea Paris. Hayo yameandikwa na gazeti la kila siku la Buenos Aires liitwalo La Nación.
Air France wameshikwa na kigugumizi juu ya habari hizo za La Nación walipohojiwa na gazeti moja la Ujerumani, Bild. Gazeti la kila siku la Paris, Le Figaro linaandika kuwa usalama kwenye viwanja vya ndege kwenye nchi za Latin Amerika ni hafifu ukilinganisha nchi za Ulaya. Kuna uvumi kuwa labda magaidi wametumia mwanya huo kupenyeza bomu ambalo limetumika kuangusha AF 447. Huo ni uvumi. Kuna nadharia nyingi zinazotolewa na wataalamu wa usalama, mambo ya anga na ”wajuaji” juu ya kupotea kwa AF 447 kwenye bahari ya Atlantiki.
Orodha ya watu na nchi wanazotoka wanaosadikiwa kufariki kwenye ajali hiyo (chanzo: Air France): Brasil: 58, Ufaransa: 61, Ujerumani: 26, Afrika Kusini: 1, USA: 2, Argentina: 1, Austria: 1, Ubelgiji: 1, Uingereza: 1, Canada: 1, China: 9, Kroatia: 1, Denmark: 1, Hispania: 2, Estonia: 1, Gambia: 1, Hungaria: 4, Ireland: 3, Iceland: 1, Italia: 9, Lebanon: 5, Morokko: 2, Uholanzi: 1, Norway: 3, Philippine: 1, Poland: 2, Romania: 1, Urusi: 1, Slovakia: 1, Sweden: 1, Uswissi: 1, Uturuki: 1
No comments:
Post a Comment