Air France yapotea kwenye
bahari ya Atlantiki
Ndege ya aina ya Airbus A330-200 ya Air France namba AF 447 yapotea kwenye bahari ya Atlantiki ikiwa na abiria 228. AF 447 ilikuwa inatoka Rio de Janeiro, Brazil kuelekea kwenye uwanja wa Charles de Gaulle mjini Paris, Ufaransa. Inasadikiwa kuwa sababu za kupotea/kuanguka kwa AF ni dhoruba ya bahari ya Atlantiki. Miongoni mwa abiria waliokuwemo kwenye ndege hiyo ni wafanyakazi watatu wa kampuni ya StatoilHydro ya Norway waliotajwa majina yao kuwa ni; Marcela Pellizon (29), Gustavo Peretti (30), Kristian Berg Andersen (37). Marcella na Gustavo ni Wabrazili, wakati Kristian Berg ni Mnorwejiani. Wanorwejiani wengine waliokuwemo kwenye ndege hiyo ni; Karsten Moholt (58) na mtoto wake Karsten Aleksander Moholt (35), Christine Badre Schnabl (34) na Alexander Bjoroy (11) aliyekuwa anasoma Clifton College Preparatory School mjini Bristol Uingereza.
No comments:
Post a Comment