Monday, June 01, 2009

Kamati ya ulinzi na usalama

iko wapi siku zote?



Kamati ya ulinzi na usalama ya Taifa ilimemfuata Regi Mengi kuhusu malumbano yake na Rostam Aziz yaliyokuwa kwenye vyombo vya habari hivi karibuni. Mbona haijamfuata Chenge, Karamagi, Msabaha, Idrissa na hata Mwakyembe na Rostam na kuwahoji kuhusu tuhuma za Ufisadi zilizo juu ya vichwa vyao?
 
Kwa nini Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Taifa haijafanyia kazi mapendekezo ya Ripoti ya Warioba au Ripoti ya Amina Chifupa ya wenye kufanya biashara za kulevya?
 
Kwa nini kamati ya Ulinzi na Usalama wa Taifa haijafanya uchunguzi na kuwaita wale wote wanaoagiza vyakula na bidhaa mbovu pamoja na maafisa wa idara za Ushuru na Kodi ambao hukagua hizo bidhaa kabla hazijaingizwa nchini?
 
Kwa nini kamati ya Ulinzi na Usalama wa Taifa haijafanya kazi kwa umakini kuhusu suala la Maalbino kutolewa kafara?
 
Kamati hii ya Ulinzi na Usalama ilikuwa wapi Watanzania walipobambikwa magari ya wizi?
 
Kamati hii ya Ulinzi na Usalama imezubaa vipi kuwa mashirika ya umma yalioingizwa ubia na wawekezaji yanadidimia kimapato na karibu kulitia hasara ya kukata na shoka Taifa? Watu kama TRL iweje tusubiri BOT waamke na kukaripia?
 
Kamati ya Ulinzi na Usalama ilikuwa wapi Richmond na Dowans zilipotuingiza mkenge achilia mbali Kiwira?
 
Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Taifa itaanza lini kufanyia kazi Ripoti ya CAG ili kuhakikisha kuwa vitendo vya uhujumu na matumizi mabaya ya fedha hayaliingizi Taifa hasara na hata kutishia thamani ya Shilingi yetu?
 
Ni UNAFIKI mtupu na ni AIBU tupu kuwa leo Kamati hii ya Ulinzi na Usalama inamrukia Mengi na kumtaka atoe maelezo, lakini haijasema inamtaka Rostam ajieleze alipotoa habari za Mengi has kuhusu akaunti za Benki kitu ambacho ni kinyume na taratibu za kibenki (Bank Secrecy Act)!
 
Simtetei Mengi na si shabiki wake, lakini ni lazima haki itendeke na sheria zifuatwe siku zote na kila wakati si pale inapotokea maslahi ya kikundi kinachojidai ni Serikali kutumia nafasi yake kisiasa kujizatiti inapoona kuwa maslahi yao yako hatarini na kuleta kisingizio cha Ulinzi na Usalama wa Taifa!

Revolutionary Right Reverend Kishoka.

 

Hii imenyofolewa kutokahttp://www.tanzanet.org/int/. Tanzanet ni Jumuiya mawasiliano ya Watanzania mtandaoni. Lazima uwe mwanachama ili uweze kusoma na kutuma jumbe.

 

Dola yaanza kumwandama Mengi

KAULI na vitendo vya Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP Limited, Reginald Mengi, zinazowagusa watu aliowaita mafisadi papa, vimemuingiza katika matata makubwa, na sasa ameanza kubanwa na vyombo vya dola, Raia Mwema imeambiwa.

Habari za uhakika kutoka serikalini zimethibitisha kwamba mara baada ya Mengi kutoa kauli iliyowataja wafanyabiashara wenzake watano kuwa ndio mafisadi papa, kumekuwa na matukio mazito ya mfululizo yanayolenga kumbana, la karibuni zaidi likiwa ni la mfanyabiashara huyo kuitwa na Kamati Ndogo ya Ulinzi na Usalama wa Taifabofya na endelea>>>>>   


No comments: