Tuesday, June 30, 2009

Airbus 310 kutoka Yemenia

yaanguka kwenye visiwa vya

Komoro ikiwa na watu 153.




Airbus 310


Ndege moja kutoka mji mkuu wa Yemen, Sanaa ikielekea Moroni, mji mkuu wa visiwa vya Komoro, imeanguka kwenye bahari ya Hindi na inasadikiwa kuwa abiria 141 (wakiwemo watoto 3) na wahudumu 11 waliokuwemo kwenye ndege hiyo wamefariki dunia. Hayo yalisemwa na makamu wa Rais wa Komoro, Idi Nadhoim.

Habari kutoka Reuters zinasema kuwa mtoto mmoja ameokolewa akiwa hai.


No comments: