Tuesday, June 09, 2009

Apple wanatoa iPhone

mpya yenye kasi kubwa




Hapa bosi wa iPhone, Scott Forestall  akitangaza aina mpya ya iPhone


Kwenye kongamano la  watengezaji wa program za TEKNOHAMA, bosi wa iPhone Scott Forestall ametangaza kuwa kampuni ya Apple itatoa hivi karibuni aina mpya ya iPhone yenye jina la iPhone 3 GS (S for speed) ambayo itakuwa na kasi zaidi ya aina za iPhone zilizo kwenye masoko. iPhone 3 GS itakuwa na uwezo wa kuianganisha na Bluetooth na USB kwenye gari, kuchukua video na kuirekebisha na kumtumia mtu, GPS ya uhakika na kuliko vyote, bei yake itaanza kwa Dala 99,- nchini Marekani.


No comments: