Thursday, June 11, 2009

Eniro yanyanua mikono juu!




Kampuni ya TEKNOHAMA ya Eniro Norway yaamua kuondoa tarehe za watu za kuzaliwa kwenye katalogi mtandao lao la simu.

http://www.telefonkatalogen.no

Eniro waliamua kuweka tarehe za kuzaliwa kwa wakazi wote wa Norway kwenye makatalogi mtandao ya simu. Mtu alikuwa akitafuta jina la mtu mwingine kwenye hilo katalogi simu mtandao, unaona jina, tarehe ya kuzaliwa, mtaa na namba za simu.

Kwa wiki moja sasa kumekuwa na kampeni bab´kubwa za wateja za kuwataka Eniro kuondoa tarehe za kuzaliwa kwenye hilo katalogi simu mtandao. Na kampeni za wateja zimezaa matunda. Eniro yanyanyua mikono juu na kuamua kusikiliza matakwa ya wateja ya kuondoa tarehe za kuzaliwa. Hayo yamesemwa na mkurugenzi wa mawasiliano wa kampuni hiyo, Bård Hammevold.

No comments: