Thursday, June 11, 2009


Idara ya usalama

jeshi la Norway (FOST)

yamchunguza Waziri Mkuu!




Idara ya usalama ya jeshi la Norway, FOST (Forsvarets sikkerhetstjeneste) imejikuta kwenye skendo ya mwaka hapa Norway. Imegundulika kuwa jamaa wa FOST wamekuwa wakichunguza ofisi ya waziri mkuu wa Norway (pamoja na waziri mkuu), Jens Stoltenberg na wizara zote, kwa kufuatilia nyendo za mawasiliano ya mtandaoni. Hiyo inawagusa watu 5000 wanaofanya kazi wizarani na ofisi ya waziri mkuu. Kugundulika huko kwa FOST kumetangazwa jana usiku kwenye taarifa ya habari ya TV 2. Yaliyofanywa na FOST hayaendani na shughuli zao.

Mnadhimu Mkuu wa jeshi la Norway, Vice Admiral Jan Eirik Finseth, emethibitisha kuwa kitengo cha polisi kinachoshughulika na uhalifu wa jinai, KRIPOS (KRIminalPOlitiSentralen) , tayari imeshaanza kuchunguza tuhuma hizo dhidi ya FOST.

Idara hiyo ambayo shughuli zake kubwa ni kuhakikisha usalama jeshini na kuwa habari za siri hazipotei njia na kwenda kusikohusika.

No comments: