Wednesday, June 24, 2009

Je, Tanzania yatishiwa

na Misri?




Mhariri wa blogu amekaa nchini Misri miezi miwili na ameandika kuhusu ”Water Resources Management in Egypt”. Moja na mambo ambayo yanaweza kuifanya Misri kupigana vita ni maji ya mto Nile. Wamisri wanasema wanaweza kuzichapa na yeyote yule atayechezea chanzo cha Mto Nile. Uhai wa wamisri unategemea sana mtiririko wa maji ya mto Nile. Bila maji ya mto Nile, hakuna taifa linaloitwa Misri. Je, Tanzania imetishiwa kushambuliwa na Misri?

*******

SERIKALI imekiri kupokea malalamiko kutoka Misri juu ya uamuzi wa Tanzania kutumia Ziwa Victoria kwa ajili ya maeneo ya Shinyanga na Mwanza na kusema hilo linajadilika. Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, jana alifanya kikao na Balozi wa Misri nchini, kujadili suala hilo ambalo linaonekana kulitia wasiwasi taifa hilo la Afrika Kaskazini.....bofya na endelea>>>>>


1 comment:

Anonymous said...

Wamanga wasitutishe...


Nitarudi nyumbani kupigana kama wakujaribu upuuzi wao na watakiona....