Friday, June 05, 2009

Kabila linaloendeleza

ukeketaji kwa wanawake


Msichana wa Kibarbaig. 

 

*Hawatambua matumizi ya kondomu,

linaongeza kwa unyanyapa


*Anayekuwa kwa UKIMWI,

huzikwa na vitu vyote alivyoacha



Na Mary Margwe



TANZANIA kama ilivyo kwa nchi nyingine duniani, ina makabila mbalimbali ambayo baadhi yake, yanazingatia mila na utamaduni wao. Miongoni mwa makabila hayo ni kabila la Wabarbaig, ambalo lipo mkoani Manyara.

Jamii ya kabila hilo inapatikana katika Wilaya za Hanang, Mbulu na Babati wakiendesha maisha yao katika maeneo ya porini na kujishughulisha na shughuli za ufugaji. Sababu kubwa iliyoifanya jamii hiyo kuishi maeneo hayo ni kuepuka kero mbalimbali ambazo wataweza kuzipata baina yao na wakulima.

Chakula maarufu kinachotumiwa na jamii ya kabila hilo ni maziwa, nyama, ugali na damu ya ng'ombe ambaye hufungwa shingoni na kupigwa kishale katika mishipa mikubwa ya damu na kukinga damu yake na kisha kuikaanga na kuila kama chakula.

Kiburudisho kinachotumiwa na kabila hilo ni pombe ambayo hufahamika kwa jina la 'Gesuda', ambayo hutengenezwa kutokana na mchanyanyiko wa asali na baadhi ya miti aina 'Harghadetcka'...bofya na endelea>>>>>  

No comments: