Monday, June 01, 2009

Kujitangaza muflisi leo



Kampuni kubwa kuliko zote za kuunda magari nchini Marekani, General Motors (GM) leo itajitangaza kufilisika. GM imekuwa katika hali ngumu ya kiuchumi, toka matatizo ya kifedha na kiuchumi yalipoanza duniani. Kwa muda mrefu GM wamekuwa wakijiendesha kwa ruzuku toka serikali kuu ya Marekani na Juni Mosi ndio siku ya mwisho waliyopewa kuwasilisha mipango ya baadaye ya jinsi GM inavyoweza kujikwamua isifilisike.

Kufuatilia sheria la kuwa muflisi ya Marekani (Chapter 11), GM italindwa na wanaowadai, hivyo itasaidia GM kuendesha shughuli za uzalishaji kwa muda

Leo Rais Obama atazungumza na taifa kuhusu maisha ya baadaye ya GM.  

No comments: