Mmisri ajikata uume
kupinga kuchaguliwa mke
Kijana mmoja Mmisri mwenye miaka 25 amejikata uume kwa kisu kupinga uamuzi wa wazazi wake kumchagulia mke. Kijana huyo alikuwa ana mpenzi wake ambaye alipanga kuoana naye, lakini wazazi wake hawakupendezewa uchaguzi wake, wakaamua kumtafutia mchumba. Kijana huyo anayetoka kwenye mji wa Sheikh Eissa kusini ya Misri, alipelekwa hospitali, lakini madaktari wameshindwa kuunganisha uume wake. Shirika la habari la Ufaransa, Agence France Presse (AFP) linaripoti.
1 comment:
Sasa huyu jamaa kamkomoa nani? Wazazi wake au mwenyewe? Maana sasa hata hataweza tena kumkidhi haja yule girl friend wake....
Post a Comment