Thursday, June 25, 2009

Kutoka Bungeni:

Mawaziri ni sawa na mbwa



Bunge la Jamhuri ya Tanzania, mjini Dodoma.


MASHAMBULIZI ya wabunge dhidi ya mawaziri bungeni, yamefikia katika hatua mbaya zaidi baada ya Mbunge wa Iramba Magharibi, Juma Kilimba (CCM), kuwafananisha na mbwa.

Kilimba aliwafananisha mawaziri na mbwa juzi usiku alipokuwa akichangia hotuba ya Waziri Mkuu ya makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2009/2010 inayotarajiwa kuhitimishwa leo.

“Mheshimiwa Waziri Mkuu, tutakunong’oneza mawaziri hawa kama mbwa, maana mbwa anamuheshimu sana anayempa chakula na si anayemtafutia chakula, wanaheshimu sana walio juu yao kikazi badala ya kuwaheshimu wananchi,” alisema Kilimba...bofya na soma zaidi>>>>>


No comments: