Henry Joseph wa Simba
Emeh Godwill (kushoto toka Naijeria) na
Henry Joseph (kulia toka Tanzania)
wakiwa kwenye uwanja wa Gjemselund wa Kongsvinger.
Kocha Tom Nordlie akiwa na Henry Joseph kwenye mazoezi ya Kongsvinger.
Mchezaji Henry Joseph wa klabu ya Simba ya Msimbazi jijini Dar es Salaam, amesajiliwa na Kongsvinger fotballklubb ya daraja la kwanza Norway (Kongsvinger haiko kwenye ligi kuu). Henry amefuzu majaribio la kuchezea Kongsvinger. Kocha wa Kongsvinger, Tom Nordlie ameridhishwa na uchezaji wa Henry. Pamoja na Henry, mchezaji Emeh Godwill toka Naijeria, naye amesajiliwa na Kongsvinger kwa msimu wa 2009/2010.
No comments:
Post a Comment