Tuesday, July 07, 2009

Sakata la mahakama

ya kadhi




Dar Leo

WAISLAMU wamesema iwapo Serikali itapuuza matakwa 12 yaliyotolewa basi itakuwa imepoteza fursa ya mwisho ya maelewano na isije ikamlaumu yeyote kwa yatakayojiri baadaye. Mbali na kukerwa na kitendo cha Serikali kuwadanganya Waislamu kuhusu mchakato wa kuwepo kwa Mahakama ya Kadhi nchini pia wamesikitishwa na kauli za Waziri wa Katiba na Sheria, Mathias Chikawe kusema bungeni kwamba Afrika Kusini ina Waislamu wengi wakati si kweli kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2007...bofya na endelea>>>>>


majira

TAMKO lililotolewa na Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA), kupinga uamuzi wa Serikali wa kukataa kuanzishwa kwa Mahakama ya Kadhi, umewashutua viongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na kulazimika kukesha wakijadili suala hilo. Habari za kuaminika ambazo gazeti hili limezipata, zimeeleza kuwa tangu juzi baadhi ya viongozi wa CCM walikuwa wakikutana mara kwa mara kujadili tamko hilo. Kwa mujibu wa vyanzo vya gazeti hili, viongozi hao wa CCM juzi walikuwa na mkutano wa kujadili msimamo wa BAKWATA uliotangazwa na Mufti wa Tanzania,Sheikh Issa Shabaan Simba, hadi usiku. Viongozi hao walifikia hatua hiyo kwa kile wanachodai kuwa tamko hilo ni sumu kali kwa kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa...bofya na endelea>>>>>

Habari Leo

SERIKALI imekutana na jopo la mashehe wa Kiislamu kupanga mfumo wa uendeshaji wa Mahakama ya Kadhi nchini, ambayo mchakato wake wa uanzishwaji unaendelea. Sambamba na hilo, Waziri Mkuu atasahihisha bungeni kauli aliyotoa Waziri wa Katiba na Sheria, Mathias Chikawe, kuwa Mahakama hiyo ya Kadhi haitakuwapo na badala yake itaingizwa kwenye sheria za nchi....bofya na endelea>>>>>

Mwananchi.

SHEIKH Mkuu wa Tanzania, Mufti Issa Shaaban bin Simba amesema kuwa hoja ya Mahakama ya Kadhi haijazikwa bali itaendelea kujadiliwa na serikali kwa msaada wa masheikh. Mufti Simba ametoa kauli hiyo baada ya serikali kutangaza Juni 30 kuwa haitaunda Mahakama ya Kadhi na badala yake itatafsiri sheria za Kiislamu na kuzijumuisha kwenye sheria za nchi ili zitumike kwenye mahakama za kawaida....bofya na endelea>>>>

Tanzania daima

MUFTI wa Tanzania, Sheikh Mkuu Issa bin Shaaban Simba, amegeuka na kuwataka waumini wa dini ya Kiislamu kuwa watulivu juu ya suala la Mahakama ya Kadhi kwa kuwa halijafa na bado linafanyiwa kazi. Kauli hiyo ya Mufti imekuja baada ya kuahidiwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kuwa hoja ya kutokuwapo kwa mahakama hiyo imefutwa bungeni....bofya na endelea>>>>>


No comments: