Thursday, July 16, 2009

Hivi unafikiri tukizeeka tutakuwa

wabinafsi na wachoyo kama hawa

wazee wa siku hizi?




Kwa Waziri wa Mikiki na Makeke,
Uzitoni Street,
Bongo.

Mpenzi wangu,

Mimi ni mzima sana ila uzima wangu wazimwa na wazimu wa kukukosa. Nimejawa na hofu na mashaka juu yako uliye mbali na macho yangu. Na ukiwa mbali nitawezaje kukufunulia moyo wangu na kukuonyesha jinsi ninavyokupenda?

Tena umesema una malaria. Jamani, pole mpenzi. Natamani kuwa karibu na wewe, nikutunze, nikudekeze kidogo, nikuandalie mapochopocho ili nikubembeleze kula. Nakujua mpenzi. Ukiwa peke yako wajidai gaaaangwe, eti hujisikii kula. Wanaume bwana, ugangwe wote wa nini wakati chakula ni dawa? Wanipa wasiwasi hivyo. Hebu kula kidogo basi kwa ajili ya mpenzi wako. Kama siwezi kuwepo angalau uniridhishe kwa kula kidogo. Kidogo mpenzi ... kidoooogo!...bofya na endelea>>>>>


No comments: