Rais Mwai Kibaki yuko
nchini kwa ziara ya
siku mbili
Rais Mwai Kibaki wa Kenya.
UHUSIANO kati ya Kenya na Tanzania uko imara na ziara ya siku mbili ya Rais Mwai Kibaki hapa nchini imezidi kuimarisha uhusiano baina ya nchi hizi mbili.
Marais Jakaya Mrisho Kikwete wa Tanzania na Rais Mwai Kibaki wa Kenya wameyasema hayo katika kikao cha pamoja kilichofanyika Ikulu ya Dar-es-Salaam, jana mchana mara baada ya kuwasili nchini.
Katika mazungumzo yao viongozi hao wawili kila mmoja alipata nafasi ya kumweleza mwenzake kuhusu hali ya kisiasa na kiuchumi ya nchi yake na Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa ujumla.
No comments:
Post a Comment