Thursday, July 09, 2009

Homa ya mafua ya nguruwe

yaingia Tanzania




Tanzania imesema kuwa mwanafunzi wa kiingereza aliyekuwa amelazwa mapema mwezi huu amethibitishwa kuwa mgonjwa wa kwanza wa homa ya mafua ya nguruwe.

Naibu Waziri wa Afya wa nchi hiyo, Dr Aisha Kigoda, amesema leo kuwa mwanafunzi huyo alikuwa miongoni mwa kundi la wanafunzi 15 waliyowasili wiki iliyopita kutoka Uingereza kwa ajili ya kazi za kujitolea.

Amesema mwanafunzi huyo aliwaambia maafisa wa uhamiaji kuwa alikuwa akijisikia vibaya ambapo alipelekwa haraka hospitalini alikogundulika kuwa na maradhi hayo ya homa ya mafua ya nguruwe.

Tanzania inakuwa nchi ya nne barani Afrika kuthibitisha kuwepo kwa mgonjwa mweye virusi vya maradhi hayo. Nyingine ni Kenya, Uganda na Ethiopea

Shirika la Afya Duniani, WHO, limethibitisha kutokea kwa vifo vya watu 429 kote duniani vilivyosababishwa na maradhi hayo ya homa ya mafua ya nguruwe, huku watu takriban elfu 95 wakiambukizwa virusi vya maradhi hayo.


No comments: