Wednesday, July 15, 2009

Makosa 10 wanawake wengi

huyafanya bila kujijua



Wataalam wa mambo ya akili wamegundua kuwa mlimbikizo wa mawazo (Stress) unaeweza kupelekea ugonjwa huu wa akili ambao humfanya mwanamke kuhisi hana thamani na suluhisho ni kuamua kusitisha maisha yake na wakati mwingine ya wale waliokaribu naye.

Kitu ambacho wanawake wengi hawatambui ni kwamba hali hii inaweza kutokea endapo utaruhusu maumivu ya moyo yatawale akili yako. Wanawake tumeumbwa na nguvu ambayo kama tutaitumia Ipasavyo, tutaishi tupendavyo… mmenisoma?

Kutoruhusu matatizo yatawale akili yako. .

Kuna makosa 10 wanawake wengi huyafanya bila kujua haya ni yakuepuka na leo niko hapa kuyachambua:-

1) KUAMINI KUPITILIZA
Ukijipa mia kwa mia kuwa hutokaa utendwe jua uko katika nafasi kubwa ya kuja kuumia kupitiliza pale utakapokuja kugundua kuwa uliyemuamini kupitiliza siye. Jenga imani kuwa kila kitu kinawezekana… kisha omba Mungu atasaidia, na hata likikufika basi umejiandaa.

2) KUWA TEGEMEZI
Unapokuwa tegemizi mara nyingi ndiye ambaye utakuja kuumia zaidi pale mambo yanapokuja kukugeukia. Kujishughulisha nako kunasaidia kupoteza mawazo kiasi fulani. Na ukweli ni kwamba kusubiri uletewe ndiko ambako kunaleta mitafaruku katika uhusiano na kupelekea kuchokwa.

3) KUKUMBATIA MATATIZO
Hakuna njia nzuri ya kuyakabili matatizo ya nyumba kama kukubali na kupiga moyo konde. Kujishusha na kuomba msamaha ikibidi. Inaweza kuwa kazi ngumu lakini ni njia nzuri ya kukuepushia maumivu zaidi natayoweza kukuondoea msongamano wa mawazo.

4) KUJITUPIA LAWAMA
Usikubali hata siku moja kujiuguza kwa maumivu ya lawama unayojipa. Jua kuwa katika kila wakati mgumu kuna kheri mbele yake. Subira ni ngumu lakini muhumu sana katika maisha ya mwanamke.

5) KUJISAHAU
Unapoamua kuweka mbele mtu mwingine zaidi yako unakuwa hujitendei haki. Mwengine anaweza kukusaliti lakini wewe huwezi kujisaliti. Ukijifunza kujipenda mwenyewe kwanza hutokonda wala kuruhusu kuumia na vitu vidogo vidogo.

6) KUJILIMBIKIZIA MAWAZO…
Wanawake wengi wanadiriki kufa na vitu kifuani mwao, jua kwamba wakati mwingine huwezi kufanya kila kitu wewe kama wewe. Tafuta msaada kwa watu wazima, uondokane na huo mzigo kifuani mwako.

7) KUJIUMIZA BILA SABABU
Unaposhindwa kufanya vitu vya maana kwa kukaa hapo kufikiria tabu za maisha yako wakati mwingine unapoteza muda wa bure. Fanya kitu tofauti na mazoea inawezakukusaidia kuona ulimwengu mwingine ambao huenda ulikuwa huujui.

8) KUFICHA MAUMIVU
Usijaribu hata siku moja kuficha maumivu wakati unaumia, tafuta njia ya kutatua matatizo yako once and for all.

9) KUWA NA NDOTO ZA ABUNUWASI
Nilishawahi kusema kuwa hakuna mwenye uwezo wa kumbadili mtu mwingine, isipokuwa mtu mwenyewe akubali kubadilika. Sasa badala ya kuungumia na namna ya kumbadili ni vyema ukakubali matokeo.

10) KUTO JITAMBUA
Ni muhimu kwa kila mwanamke kutambua na kuelewa kuwa yeye ni kiumbe muhimu katika jamii. Yeye ndiye muongozo wa kizazi kijacho. Yeye ndiye tumaini. Kwa kutoruhusu matatizo yatawale akili yako, utasevu maisha yako na ya wale wanaokutegemea.

Kutoka kwa dada Asmah, gazeti la Mwananchi.


No comments: